HAWA NDIO WATU MAARUFU WALIOFARIKI KWENYE WESTGATE MALL NCHINI KENYA
Ruhila aliolewa mwaka jana
Takriban
watu 62 wameuawa kwenye mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya dhidi ya
jengo la kifahari lenye maduka zaidi ya themanini la Westgate.
Ruhila Adatia-Sood
Ruhila Adatia-Sood na mumewe Ketan Sood Ruhila Adatia-Sood walioana tu mwezi Januari mwaka jana.
Ruhila,
alikuwa katika ghorofa ya juu ya duka la Westgate ambako alikuwa
miongoni mwa watu waliokuwa wameandaa mashindano ya upishi kwa watoto.
Alikuwa
ameolewa na Ketan Sood, aliyefanya kazi na shirika la USAid mjini
Nairobi mwezi Januari mwaka 2012,na harusi yake ilitajwa kuwa harusi ya
kiswahili ambayo ilisherehekewa kwa siku tatu.
Alikuwa mjamzito na mimba ya miezi sita alipofariki.
Kulingana na ripoti Adatia-Sood alikimbizwa hospitalini , lakini alifariki baada ya kuwasili kutokana na kuvuja damu nyingi.
Alisifika kote nchini kwa moyo wake mzuri wa kuwafanya watu kutabasamu daima.
Polisi wakikabiliana na wanamgambo hao waliokuwa wameteka jengo la Westgate
Kwenye ukurasa wake wa Twitter alijitaja kuwa mpenda chakula na mtu mwenye kufurahia michezo ya kusisimua.
Alisomea katika chuo kikuu cha Rhodes nchini Afrika Kusini , na dada zake watatu wamemtaja kama mtu mwenye ari kubwa maishani.
Pia alikuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha East FM na pia alitangaza habari kwenye kituo cha televisheni ya Kiss.
Magaidi
waliwarushia magurunedi Rahila na mtangazaji mwenzake pamoja na watoto
waliokuwa ndani ya jengo hilo lakini Ruhila hakuponea. Mwenzake Kamal
Kaur, pia mtangazaji wa redio alikuwa ameambatana na watoto wake ambao
walifyatuliwa risasi ingawa ziliwakosa na kumgonga mtoto aliyekuwa
karibu nao. Wao walijeruhiwa miguuni.
Kaur na wanawe walifanikiwa kukimbilia usalama wao.
Mbugua Mwangi and Rosemary Wahito
Rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta pia aliwapoteza jamaa zake katika shambulizi hilo.
Mbugua Mwangi ni mpwa wa Kenyatta na alikuwa na mchumba wake Rosemary
Wahito wakati waliposhambuliwa kwa risasi na kuuawa papo hapo.
Akihutubia
taifa, Kenyatta alisema kuwa, "ninamuomba Mungu awape utulivu wakati
sote tukikumbwa na msiba huu na ninajua mnachokihisi hasa ikiwa
umempoteza jamaa wako katiakshambulizi hili baya.''
Kulingana
na taarifa ya jarida la nchini Ireland, mamake Mwangi, Catherine Muigai
Mwangi, ndio alikuwa tu amerejea kutoka Dublin ambako alikuwa balozi wa
Kenya kwa miaka sita .
Dadake mkubwa Rais Kenyatta Christine Wambui Pratt pia alikuwa katika jengo hilo lakini alifanikiwa kunusuru maisya yake.
Mitul Shah
Mitul Sha alipenda sana soka
Mitul Shah Mitul Shah alikuwa mkuu wa timu ya soka ya kampuni yake ambayo inacheza katika divisheni ya pili.
Afisaa
mkuu mtendaji wa mauzo katika kampuni ya Bidco, ambayo hutengeza mafuta
ya kupikia, Mitul Shah alikuwa katika ghorofa ya juu zaidi ya jengo
hilo.
"Alifariki akijaribu kuwaokoa watoto waliokuwa wamekwama ndani ya jengo hilo. Kwa marafiki wa Mitul, alifariki kama shujaa .
Rafiki zake wamemtaja kama shabiki sugu wa Manchester United.
Pia alikuwa mwenyekiti wa timu ya soka ya Bidco.
Joyti Kharmes Vaya na Maltiben Ramesh Vaya ambao ni wifi
Mazishi ya Joyti Kahrmes Vaya na Maltiben Ramesh Vaya
Joyti
Kharmes Vaya alikuwa na umri wa miaka 37 mwenye watoto watatu, ambaye
mumewe alifanya kazi katika benki ya Victoria Commercial bank.
Maltiben Ramesh Vaya alikuwa na miaka 41 , mama wa watoto wawili aliyefanya kazi katika Benki ya Baroda.
Wawili hao walikufa kutokana na majeraha waliyopata, kutoka na risasi
Kofi Awoonor
Raia wa
Ghana mwenye umri wa miaka 78 malenga anayesifika sana. Anasifika
nyumbani kwao kama mwandishi ambaye vitabu vyake vinatumiwa katika shule
nyingi nchini Ghana.
Alikuwa mjini Nairobi kushiriki hafla ya Storymoja na alitarajiwa kutumbuiza watu siku ya Jumamosi.
Alisifika kwa nyimbo na mashairi yake mapema miaka ya sitini.
Miaka ya
sabini alifunza katika baadhi ya vyuo vikuu nchini Marekani na kurejea
Ghana mwaka 1975 kuchukua wadhifa wa mwalimu wa lugha ya kiingereza
katika chuo kikuu cha Cape Coast.
Katika
muda wa miezi kadhaa, alikamatwa na kuzuiliwa kwa madai ya njama ya
uhaini wakati wa utawala wa kijeshi wa Kanali Ignatius Acheampong.
Mwanawe
Awoonor alikuwa naye wakati wa shambulii hilo mjini Nairobi na alipigwa
risasi mkononi wakati wa shambulizi hilo













0 comments: